Job 27:1-6

Ayubu Anadumisha Uadilifu Wake

1 aNdipo Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema:
2 b“Hakika kama Mungu aishivyo, aliyeninyima haki yangu,
Mwenyezi ambaye amenifanya
nionje uchungu wa nafsi,

3 ckwa muda wote nitakaokuwa na uhai ndani yangu,
nayo pumzi ya Mungu ikiwa puani mwangu,

4 dmidomo yangu haitanena uovu,
wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.

5 eSitakubaliana nanyi kabisa kuwa mko sahihi;
hadi nife, sitakana uadilifu wangu.

6 fNitadumisha haki yangu wala sitaiacha;
dhamiri yangu haitanisuta muda wote ninaoishi.

Copyright information for SwhKC